ofisa wa Upelelezi Mbozi akionyesha
sehemu ya Mbolea mbovu ambayo
imefumbiwa macho na Mamlaka
ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na
kuitakatisha kama haina matatizo
wala madhara kwa wakulima
Katika hali inayoonyesha kuna mchezo
mchafu wa kuendelea kuwamaliza
wakulima wilayani Mbozi, shehena ya
Mbolea mbovu iliyozuiwa kuuzwa
mwaka jana hatimaye “upepo umepita”
na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu kiviwango!
Katika hali hiyo wakulima wamekuja
juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi
wa duka la STACCO ambalo miezi kadhaa
lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na
kwa mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa
vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa
kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa,
likafuata la pili na hatimaye la tatu!
Wakati wananchi kwa macho yao meupe
wakishuhudia mifuko iliyoganda ya
Mbolea za UREA, DAP, CAN na SA
taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa
kwa duka hilo inatoa maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu! ambayo ni mifuko 11 tu.
Hata hivyo afisa anayesimamia ubora wa
Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya
Mbozi Bi Shonyela amesema licha
ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka
kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza
wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa
Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.
“nimeandikiwa Mbolea aina ya SA pekee
ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa
polisi kwenda Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu!
Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni zaidi ya
mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa
imekuwa kimya” alifafanua
Uchunguzi wa haraka kwenye duka hilo
unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa
imeganda wakati wa kufunga duka hilo mwezi
September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11 na SA 11.
Ingawa katika maelezo ya mkurugenzi
wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbole
a Tanzania TFRA ilionyesha kuwa wangeshirikiana
bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha
viwango vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP, CAN na UREA
iliyoharibika kwenye ghala la STACO
wilayani Mbozi yanajenga mawimbi na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa macho!
Tanzania hutegemea maabara yake ya
Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga
kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa
serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na
makampuni yanayofanya shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika mzunguko wa fedha nchini
Wakati pia chuo cha kilimo SUA
kimekuwa kikitumika katika tafiti na
uchunguzi wa Mbolea, mwaka jana
Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika
Dr Adam Malima alikataa matokeo ya
uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na
SUA na kuahidi sampuli za Mbolea
iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa maabara za huko baada
ya kulalamikiwa na wakulima
Aidha naibu waziri alisitisha leseni za
makampuni ya STACO na Mohamed
Enterpries mnamo August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye duka la STACO
“Maamuzi ya mamlaka ya ukaguzi wa
ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi wakikosa imani kutokana na namna maamuzi
yanavyofikiwa hata katika mambo
ambayo hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza bwana Keneth Mwazembe
mmoja wa wakulima wakubwa wilayani Mbozi.
Msimamizi wa duka la STACO bwana
Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea
ambayo haimo kwenye barua ya kuruhusu
uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo
Ni kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea
mchanganyiko ambayo ni mbovu na tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius Masai
Duka hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!
Kwahisani ya Indaba Africa
|
No comments:
Post a Comment
Asante kwa maoni yako. Karibu tena