Mafundi hawa wakiendelea na ujenzi wa hali ya juu sana kwa ajili ya kuboresha barabara inayo elekea katika Hospitali ya Mbozi Mission
Kila mtu kwa nafasi yake hapa anapiga mzigo, Madogo pia wamo ilikuwa ni siku ya weekend
Hii Ndiyo hali Halisi ya Daraja hili
Daraja hili lilikuwa ni la muda ambapo ujenzi unaendelea pembeni
Ukicheki Barabara imetulia Lakini ukitazama na Daraja pia Limetulia kwa kiwango cha juu sana hizi ni Juhudi za wilaya ya Mbozi kufanikisha mambo ya miundo mbinu
Hii ni moja ya Lami yenye kiwango cha juu sana, inatoka Dar es salaam mpaka Tunduma, Hapa ni Ihanda Mbozi Tanzania
Daraja la Juu na la chini ni moja ya madaraja imala ambayo yapo njia moja huko katikati ya vijiji kabisa
Kama unavyo onekana ujenzi hapa ni Barabara ya Ndolezi kuelekea katika kimondo ikiwa inaboreshwa kwa kuwekewa ma Kalavati mapya kabisa
Hili Ni Kalavati jipya ambalo limepita katikati ya Barabara ya kuelekea Ndolezi katika Kimondo
Hii Ni moja ya Njia ambazo zimenyooka sana na ubora wa kiwango cha Juu sana
PICHA ZOTE NA BLOG YA WILAYA YA MBOZI
Nashukuru kwa kutuhabarisha lakini pia jaribu kugusa nyanja mhimu kama kilimo cha kahawa ambacho ni mhimili wa uchumi wa wilaya. Wakulima waelimishwe kupitia mtandao huu namna ya kuboresha zao hili na jinsi ya kutafuta masoko nje badala ya kutegemea mnada wa Moshi. Mi kama mtaalam wa kilimo nikiwa nimebobea katika huduma za agronomia ya kahawa na uboreshaji wa kahawa nipo tayari kusaidia kuelimisha wakulima wetu pale Mbozi kama nitaalikwa rasimi na mtandao huu.
ReplyDelete