Social Icons

Pages

Featured Posts

Friday, 26 April 2013

HIVI NDIVYO WANANCHI MBOZI WALIVYO LIZWA NA MBOLEA FEKI,SOMA HAPA


 Sehemu ya Mifuko ya Mbolea kimeo ikisogezwa
 pembeni na vijana wa kazi baada ya kufunguliwa 
kwa dula la Mbolea la STACO LTD na
 kusafishwa kwamba mbolea nyingine haina matatizo

 Mbolea yenye alama ya kampuni ya 
YALA aina ya DAP ambayo pia imekutwa ikiwa chini ya kiwango

ofisa wa Upelelezi Mbozi akionyesha 
sehemu ya Mbolea mbovu ambayo
 imefumbiwa macho na Mamlaka 
ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na
 kuitakatisha kama haina matatizo
 wala madhara kwa wakulima


Katika hali inayoonyesha kuna mchezo
 mchafu wa kuendelea kuwamaliza 
wakulima wilayani Mbozi, shehena ya 
Mbolea mbovu iliyozuiwa  kuuzwa 
mwaka jana hatimaye “upepo umepita” 
na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu kiviwango!

Katika hali hiyo wakulima wamekuja
 juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi
 wa duka la STACCO ambalo miezi kadhaa
 lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na
 kwa mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa
 vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa 
kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa,
 likafuata la pili na hatimaye la tatu!

Wakati wananchi kwa macho yao meupe
 wakishuhudia mifuko iliyoganda ya
 Mbolea za UREA, DAP, CAN na SA
 taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa 
kwa duka hilo inatoa maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake  ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu! ambayo ni mifuko 11 tu.

Hata hivyo afisa anayesimamia ubora wa
 Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya
 Mbozi Bi Shonyela amesema licha 
ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka
 kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza 
wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa 
Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.

“nimeandikiwa Mbolea aina ya SA pekee
 ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa 
polisi kwenda Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu! 
Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni zaidi ya
 mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa
 imekuwa kimya” alifafanua

Uchunguzi wa haraka kwenye duka hilo 
unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa
 imeganda wakati wa kufunga duka hilo mwezi
 September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11 na SA 11.

Ingawa katika maelezo ya mkurugenzi 
wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbole
a Tanzania TFRA ilionyesha kuwa wangeshirikiana
 bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha 
viwango vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP, CAN na UREA
 iliyoharibika kwenye ghala la STACO 
wilayani Mbozi yanajenga mawimbi na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa macho!

Tanzania hutegemea maabara yake ya
 Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga
 kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa 
serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na 
makampuni yanayofanya shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika mzunguko wa fedha nchini

Wakati pia chuo cha kilimo SUA
 kimekuwa kikitumika katika tafiti na 
uchunguzi wa Mbolea, mwaka jana
 Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika
 Dr Adam Malima alikataa matokeo ya
 uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na
 SUA na kuahidi sampuli za Mbolea
 iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa maabara za huko baada 
ya kulalamikiwa na wakulima

Aidha naibu waziri alisitisha leseni za
 makampuni ya STACO na Mohamed 
Enterpries mnamo August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye duka la STACO

“Maamuzi ya mamlaka ya ukaguzi wa
 ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi wakikosa imani kutokana na namna maamuzi 
yanavyofikiwa hata katika mambo
 ambayo hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza bwana Keneth Mwazembe
 mmoja wa wakulima wakubwa wilayani Mbozi.

Msimamizi wa duka la STACO bwana 
Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea
 ambayo haimo kwenye barua ya kuruhusu
 uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo

Ni kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea
 mchanganyiko ambayo ni mbovu na tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius Masai

Duka hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!

Kwahisani ya Indaba Africa

Friday, 28 September 2012

HAYA NDIYO MAMBO USIYO YAFAHAMU KUTOKA MBOZI .. SEHEMU YA KWANZA

 Mmea huu unatumika kutengenezea vitu kama Togwa
Alizeti zikiwa zimeshamili vizuri kabisa
 Hii Ni mboga ya Majani ya Maharage ikiwa inakaushwa

 Moja ya vitu vinavyo tengenezwa Mbozi
 Hiki ni chungu asilia Cha Mbozi
Chakula  Cha mbozi huwezi tamani kuacha kula

Tuesday, 25 September 2012

Wilaya ya Mbozi inazidi kusonga Mbele kwa kuwa na Miundo mbinu Bora na kuboresha zaidi.

 Mafundi hawa wakiendelea na ujenzi wa hali ya juu sana kwa ajili ya kuboresha barabara inayo elekea katika Hospitali ya Mbozi Mission
 Kila mtu kwa nafasi yake hapa anapiga mzigo, Madogo pia wamo ilikuwa ni siku ya weekend
 Hii Ndiyo hali Halisi ya Daraja hili
 Daraja hili lilikuwa ni la muda ambapo ujenzi unaendelea pembeni

 Ukicheki Barabara imetulia Lakini ukitazama na Daraja pia Limetulia kwa kiwango cha juu sana hizi ni Juhudi za wilaya ya Mbozi kufanikisha mambo ya miundo mbinu 
 Hii ni moja ya Lami yenye kiwango cha juu sana, inatoka Dar es salaam mpaka Tunduma, Hapa ni Ihanda Mbozi Tanzania 

 Daraja la Juu na la chini ni moja ya madaraja imala ambayo yapo njia moja huko katikati ya vijiji kabisa 
 Kama unavyo onekana ujenzi hapa ni Barabara ya Ndolezi kuelekea katika kimondo ikiwa inaboreshwa kwa kuwekewa ma Kalavati mapya kabisa
 Hili Ni Kalavati jipya ambalo limepita katikati ya Barabara ya kuelekea Ndolezi katika Kimondo
Hii Ni moja ya Njia ambazo zimenyooka sana na ubora wa kiwango cha Juu sana

PICHA ZOTE NA BLOG YA WILAYA YA MBOZI
 

Sample text

Sample Text

Sample Text